Jumanne 17 Februari 2026 - 10:26
Ramadhani ni shule ya kujijenga na jihadi ya ustaarabu

Hawza/ Ayatullah Abbas Kaabi, katika mkutano wa wakurugenzi na walinganiaji wa nchi Iran ulioratibiwa mahsusi kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani 1447 Hijria, uliofanyika kwa juhudi za muungano wa kitaifa wa makundi ya ulinganiaji katika Ofisi Kuu ya Ulinganiaji wa Kiislamu ya mkoa wa Qum Iran, alieleza huku akirejelea umuhimu wa nafasi ya ulinganiaji katika mfumo wa fikra za Uislamu: Ni jambo la kufurahisha kupata tawfiki ya kuwa karibu na mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na makundi ya ulinganiaji na kusikiliza ripoti zenye matumaini.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Kaabi alisema: Ulinganiaji una asili ya kijamii na wanazuoni wa dini pia wana utambulisho wa kijamii,” na akaongeza: Uhusiano wa wanazuoni wa dini na watu ni kama uhusiano wa samaki na bahari; ikiwa wanazuoni wa dini watatengana na watu au kukatokea umbali kati yao, hawataweza kuendelea kuishi. Kwa upande mwingine, watu pia bila wanazuoni wa dini hupata madhara makubwa katika utambulisho wao wa kidini.

Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum aliendelea kusema: Uhusiano wa wanazuoni wa dini na watu ni uhusiano unaomjenga mwanadamu, unaounda jamii, unaotoa utambulisho, unaoleta matumaini na unaofungua upeo.

Mtazamo wa jihadi na wa pamoja; faida ya makundi ya ulinganiaji

Ayatullah Kaabi akirejelea sifa za makundi ya ulinganiaji wa kijihadi alisema: Makundi haya yako hatua moja mbele, kwa sababu yanafuatilia ulinganiaji si kwa vipindi maalumu tu, bali kwa utambulisho wa pamoja, kitaaluma katika mwaka mzima. Mtazamo huu wa kijihadi katika ulinganiaji ni faida kubwa. Alisisitiza kuiga mwenendo wa Mtume Mtukufu (s.a.w.) na kusema: Uhalisia wa muhubiri na mafanikio yake hupata maana katika kuendeleza harakati ya ulinganiaji ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.ww.). Mtume Mtukufu alikuwa na sifa zilizofanya ulinganiaji wake kuwa na athari: kwanza, alikuwa kutoka miongoni mwa watu na kwa ajili ya watu; pili, alihisi kwa undani maumivu na mateso ya watu; tatu, alijitahidi kutatua matatizo yao; na nne, alitenda kwa huruma na upole, na ulinganiaji wake haukuwa wa kinadharia tu bali uliambatana na utatuzi wa matatizo.

Umuhimu wa sosholojia na utambuzi wa matatizo katika ulinganiaji

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi alisema; makundi ya ulinganiaji yanapaswa kuimarisha sifa hizi ndani yao: hatua ya kwanza ni kuijua jamii kwa usahihi na saikolojia ya walengwa. Muhubiri anapaswa kuendana na watu.
Hatua ya pili ni kutambua na kuorodhesha maumivu na matatizo ya watu, na hatua ya tatu ni kujitahidi kutoa huduma ya kweli sambamba na ulinganiaji.

Aliendelea kusema: Kuhamasisha uwezo wa mfumo, viongozi na taasisi katika kuwahudumia watu wakati wa shughuli za ulinganiaji kunaweza kugeuza kundi la jihadi kuwa mkusanyiko unaoleta mageuzi, kiasi cha kuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kijamii na hata kisiasa na kuanzisha mkondo wa kitaifa.

Imam Musa Sadr; kielelezo cha ulinganiaji unaolenga matatizo

Ayatullah Kaabi alirejelea mfano wa ulinganiaji wenye mafanikio na kusema: Imam Musa Sadr, aliyekulia katika familia ya marjaiya ya kidini, aliichunguza jamii ya Lebanon na kugundua kuwa Mashia wa nchi hiyo walikuwa wanakabiliwa na umaskini, kubaki nyuma na kudharauliwa. Baada ya kuwasili Lebanon, alianza kazi si kwa hotuba bali kwa kuanzisha shule za ufundi kwa vijana, akawahamasisha kujifunza ujuzi na ujasiriamali. Aliweka msingi wa kuondoa umaskini na wakati huo huo akaendelea na ulinganiaji wa dini. Hatua hii ilisababisha kuanzishwa kwa taasisi kama Baraza Kuu la Kishia la Lebanon na kuthibitisha utambulisho na nafasi ya kijamii ya Mashia.

Alisema pia: Watu wengi mashuhuri wa harakati za muqawama walilelewa katika shule ya Imam Musa Sadr; miongoni mwao ni aliyekuwa akisimulia kwamba alipokuwa kijana, alipoona picha ya Imam Musa Sadr katika duka la baba yake alipata msukumo na akatamani kuwa kama yeye.

Muhubiri anaweza kuwa msukumo wa taifa

Ayatullah Kaabi alisisitiza kwamba: Muhubiri anaweza kuanza kutoka kijiji au kundi maalumu, lakini kwa ikhlasi, mipango, utambuzi wa matatizo na huduma ya kweli, anaweza kuwa mfano wa kitaifa na hata msukumo kwa taifa. Makundi ya ulinganiaji yanapaswa kuthamini fursa hii na katika mwezi wa Ramadhani yaambatanishe ulinganiaji na huduma kwa jamii, mshikamano na utatuzi wa matatizo ya watu.

Alisema: “Ulinganiaji unaoambatana na ikhlasi huleta baraka.” Muhubiri anayefanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa lengo la kupata radhi za Imam wa Zama (a.f.) hataki sifa wala kutafuta kujulikana, bali ni mwenye kuwajibika, wa kijihadi na mtumishi mnyenyekevu kwa Mashia wa Amirul-Muuminina (a.s.).

Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum aliongeza: Ikiwa ulinganiaji utakuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa nia ya kupata radhi za Imam wa Zama (a.f.), bila shaka utakuwa na baraka na athari zake zitadumu.

Sifa za ulinganiaji wa kimungu Alisema: Sifa ya kwanza ni kwamba muhubiri hataki sifa wala kujionyesha, na hata akisemwa vibaya hatarudi nyuma katika njia ya kutoa huduma. Muhubiri wa kimungu ana roho ya ushirikiano, ni mwenye kuwajibika na wa kijihadi, anajiona kuwa na deni kwa Uislamu na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.), na lengo lake ni kuwahudumia Mashia wa Amirul-Muuminina (a.s.).

Ramadhani; shule ya kujijenga na jihadi ya ustaarabu

Ayatullah Kaabi aliutaja mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni “shule ya kujijenga, kuijenga jamii katika jihadi ya ustaarabu, subira na kuzalisha nguvu ya Kiislamu,” na kusema katika mwezi huu lazima kujitahidi kuunda jamii ya waumini iliyo hai, yenye uelewa, yenye subira na mtazamo wa baadaye. Alisema katika zama za Mtume (s.a.w.w) Waislamu hawakuwa katika kiwango kimoja: baadhi walitafuta maisha ya kawaida, baadhi waliathiriwa na unafiki, na baadhi hawakukata mahusiano yao na wasiokuwa Waislamu; lakini kulikuwa na kundi la waumini mashujaa na wapiganaji waliokuwepo uwanjani ambao Uislamu ulisonga mbele kupitia wao.

Aliongeza: Kiongozi wa hawa waliokuwa mbele alikuwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) na baada yake Imam Ali (a.s.). Leo pia lazima kuwapanga na kuwaandaa watangulizi wa harakati ya Uislamu halisi na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.).

Umma wa Mapinduzi ya Kiislamu; nguvu ya madhehebu

Akirejelea matukio ya hivi karibuni nchini Iran alisema: Kinachotokea kila tarehe 22 Bahman ni kudhihiri kwa “umma wa waumini” katika zama za ghaiba. “Umma wa Mapinduzi ya Kiislamu” si watu wote tu, bali ni mwili imara, unaozalisha nguvu na unaosimama uwanjani kwa ajili ya Uislamu na Ahlul-Bayt (a.s.). Alisema adui analenga kupambana na Uislamu, madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.), majlisi za Imam Husain (a.s.) na mikusanyiko ya Qur’ani; hivyo ni lazima kutumia uwezo wa ulinganiaji kumlea mwanadamu muumini mpiganaji na kuijenga jamii imara.

Qur’ani kama mhimili na kujenga mitandao ya Kiimani

Alisisitiza umuhimu wa Qur’ani katika shughuli za ulinganiaji na kusema: Qur’ani inapaswa kuwasilishwa kwa lugha ya kisasa ili kila Mwislamu aweze kupata mwongozo wa maisha ndani yake. Miradi kama “Maisha pamoja na Aya” ina uwezo mzuri kwa makundi ya jihadi.

Alionya dhidi ya urasimu katika makundi ya ulinganiaji na kusisitiza fikra ya kibasiji: kusimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, jihadi endelevu, utii kwa uongozi, kuunganisha imani na malengo, na kuwa pamoja na watu.

Alisisitiza tena tofauti kati ya ulinganiaji wa jadi na ulinganiaji wa kijihadi: katika ulinganiaji wa kijihadi ni lazima kuunda uhusiano wa kudumu na walengwa na kuwageuza kuwa mtandao wa kijamii wa Kiimani; walengwa hawapaswi kuachwa baada ya kumalizika kwa shughuli za ulinganiaji.

Alisema: Ikiwa makundi ya ulinganiaji yataandaliwa kwa fikra ya kijihadi, yatakuwa mfano wa jihadi kubwa ya fikra na ustaarabu, na yataweza kubadili udhaifu kuwa nguvu na changamoto kuwa matatizo yaliyotatuliwa.

Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisisitiza kuwa; mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya kipekee ya kuandaa umma wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuimarisha uhusiano wa imani, vitendo, jihadi na huduma katika jamii. Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi alipendekeza makundi ya ulinganiaji yaache mtazamo mdogo wa tauhidi na kuelekea katika kujenga utambulisho wa kijamii na uelewa wa kina wa dini.

Mihimili mitano ya ulinganiaji wenye athari Alitaja mihimili hii:

1. Kufafanua misingi ya tauhidi na utambulisho.
2. Kulea mwanadamu mpiganaji aliye uwanjani.
3. Kujenga jamii ya Qur’ani na mfumo wa Kiislamu.
4. Kuimarisha roho ya mapambano na subira.
5. Kuimarisha uhusiano wa umma na Uimamu.

Alisema; tauhidi lazima ionekane katika haki ya kijamii, kupunguza tofauti za kitabaka, kusaidiana, kupambana na ufisadi, na kuimarisha mema na kukataza maovu.
Pia alisisitiza kuwa mapambano dhidi ya Marekani yanapaswa kuelezwa kwa mtazamo wa tauhidi, kwamba nguvu ya kweli ni ya Mwenyezi Mungu na nguvu za kibabe hazidumu.

Umuhimu wa uhusiano wa umma na Imamu

Alisema ikiwa umma katika zama za ghaiba umtafuata Imam utafanikiwa, lakini ukitengana nae hata ibada za mtu binafsi hazitatosha.

Mwisho, Ayatullah Kaabi aliomba kuharakishwa kudhihiri kwa Imam wa Zama (a.f.) na kumjomba Mwenyezi Mungu awafanye watu wawe karibu na Qur’ani na Ahlul-Bayt (a.s.) na awape tawfiki ya kutekeleza wajibu katika jihadi ya kubainisha haki na kuutumikia Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha